Ligi ya Mabingwa barani ulaya imerudi!
Wikiendi ya soka imekuwa ya kushangaza! Liverpool walichelewa kufunga lakini wakaondoka na pointi 3 zote dhidi ya Burnley waliopanda daraja, kwa mkwaju wa penalti kutoka Mo Salah. Man City waliwabamiza mahasimu wao Man Utd kwa ushindi wa 3-0, na Haaland sasa ana magoli 7 na asisti 2 ndani ya siku 7 pekee – je, ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani kwa sasa? Takwimu zake zinaonesha hivyo. Italia, Juventus waliibuka na ushindi wa kusisimua wa 4-3 dhidi ya Inter.
Ligi ya Mabingwa barani ulaya imerudi!
JUMATANO:
BAYERN v CHELSEA
Chelsea hawajawahi kuifunga Bayern tangu 2005 na hawajawahi kushinda nchini Ujerumani. Bayern wamefunga magoli 11 katika mechi 4 za nyumbani dhidi ya Chelsea, huku Chelsea wakifunga 7 katika mechi hizo. Tegemea mchezo wa kukata na shoka!
Mashambulizi ya Bayern yakiongozwa na Kane, Diaz, na Olise ni miongoni mwa yenye hatari zaidi Bundesliga, wakiwa na jumla ya magoli 11 na asisti 6 ndani ya mechi 3 pekee. Chelsea kupitia Joao Pedro na Enzo Fernandez pia wameonyesha makali katika Premier League, wakichangia magoli 4 na asisti 4 kati yao ndani ya mechi 4.
USHAURI WA BASHIRI: Kane afunge magoli 2 au zaidi na Bayern kushinda
LIVERPOOL v ATLETICO MADRID
Mabingwa wa Premier League msimu uliopita tena wako kileleni mwa msimamo! Wameshinda mechi 4 kati ya 4, wakifunga magoli 9 lakini pia wamefungwa 4! Wakati huo huo Atletico hawajaanza vyema La Liga wakiwa na ushindi 1 pekee kwenye mechi 4, sare 2 na kipigo kimoja, wakifunga magoli 5 lakini wakifungwa 3. Kwa kuwa timu zote zina udhaifu wa ulinzi, tegemea magoli!
USHAURI WA BASHIRI: Salah afunge, timu zote zifunge, na Liverpool washinde
ALHAMISI
MAN CITY v NAPOLI
Habari kubwa kwenye mchezo huu ni gwiji wa Man City, Kevin De Bruyne, kurudi Etihad akiwa na timu yake mpya, Napoli! Kiungo huyu wa Kibelgiji yupo kwenye kiwango bora, tayari amefunga magoli 2 kwa Napoli na kuisaidia nchi yake wiki iliyopita kwa magoli 3 na asisti moja. Mchezaji bora wa Serie A msimu uliopita, Scott McTominay, pia atakutana na mahasimu wake wa zamani—je, ataweza kuleta tofauti? Mabingwa wa Serie A, Napoli, wako kileleni mwa ligi yao na ushindi wa mechi 3 kati ya 3, huku Man City wakiwa na ushindi 2 na vipigo 2 msimu huu. Licha ya hayo, Haaland amekuwa moto, akifunga magoli 5 kwenye mechi 4. City wameshinda mikikimikiki 2 ya mwisho dhidi ya Napoli—ni nani ataibuka mshindi safari hii?
USHAURI WA BASHIRI: Haaland na McTominay wafunge muda wowote.
NEWCASTLE v BARCELONA
Timu hizi zimekutana mara 4, Barcelona wakishinda mara 3 za mwisho, huku ushindi pekee wa Newcastle ukiwa mwaka 1997. Newcastle wameanza msimu vibaya, huku Issak akikataa kucheza na kusukuma uhamisho kwenda Liverpool. Wameshinda mechi 1 pekee kati ya 4, wakifunga magoli 3 tu. Mrithi wake, Nick Woltemade, alifanya tofauti mara moja kwa kufunga katika mechi yake ya kwanza—je, ataweza kuziba pengo hilo? Kwa upande mwingine, Barcelona wanapaa juu. Wameshinda mechi 3 kati ya 4 msimu huu na kufunga jumla ya magoli 13. Kijana staa Lamina Yamal alikosa ushindi wa 6-0 dhidi ya Valencia lakini anatarajiwa kurejea, akiwa na rekodi ya magoli 6 na asisti 6 kwenye mashindano yote msimu huu.
USHAURI WA BASHIRI: Barcelona kushinda, Yamal afunge muda wowote, na timu zote kufunga.
Ligi ya Mabingwa imerudi wiki hii, ikiahidi magoli ya kuvutia, msisimko, na burudani ya kukufanya usiketi vizuri kwenye kiti. Weka bashiri zako, pumzika, na ufurahie mchezo!


