Ligi Kuu ya England Liverpool vs Everton
Derby ya Merseyside, moja ya mechi kali zaidi na yenye ushindani mkubwa katika Soka la Dunia, inatarajiwa kuwasha moto tena katika Ligi Kuu ya England huku Liverpool iki-ikaribisha Everton katika uwanja wa Anfield. Mchuano huu wa kusisimua unatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa, hisia kali, na ushindani mkali ambao umeifanya mechi hii kuwa ya ki-historia.
Katika Derby 10 zilizopita za Merseyside kwenye Anfield, Liverpool imeonyesha ubabe wake kwa kushinda mechi 7, huku Everton ikifanikiwa kushinda mara moja tu, na michezo miwili kumalizika kwa sare. Je, Liverpool itaendelea kutawala na kusogea karibu zaidi na ubingwa wa ligi, au Everton itainuka na kutoa kauli thabiti katikati ya jiji la Liverpool?
Takwimu za Liverpool:
Nafasi: ya 1 kwenye Ligi Kuu
Rekodi: Ushindi 21, Sare 7, Kipigo 1 (Pointi 70)
Magoli yaliyofungwa: 69 (Wastani wa 2.38 kwa mechi)
Magoli yaliyofungwa dhidi yao: 27 (Wastani wa 0.93 kwa mechi)
Liverpool inafurahia msimu mzuri chini ya kocha Arne Slot, wakiwa vinara wa ligi kwa pointi 70. The Reds wamekuwa imara bora zaidi nyumbani, wakishinda mechi 11 kati ya 14 wali-zocheza Anfield, huku wakitoka sare mara 2 na kupoteza 1 pekee.
Takwimu za Everton
Nafasi: ya 15 kwenye Ligi Kuu
Rekodi: Ushindi 7, Sare 13, Vipigo 9 (Pointi 34)
Magoli yaliyofungwa: 32 (Wastani wa 1.11 kwa mechi)
Magoli yaliyofungwa dhidi yao: 36 (Wastani wa 1.24 kwa mechi)
Chini ya kocha David Moyes, Everton ipo kwenye mfululizo wa kutopoteza mechi, baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wao wa hivi karibuni wa Ligi Kuu. Msururu huu wa michezo tisa bila kupoteza unawapa matumaini makubwa kuelekea Derby hii muhimu.
Wachezaji Muhimu wa Liverpool
Mohamed Salah: “”Mfalme wa Misri”” amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, aki-funga mabao 27 na kutoa asisti 17 katika Ligi Kuu. Pia, ana rekodi nzuri dhidi ya Everton, akifunga mabao 8 na kutoa asisti 2 katika mechi 12 za ligi dhidi ya wapinzani wao wa Merseyside.
Wachezaji Muhimu wa Everton
·Beto: Mshambuliaji huyu ameweka rekodi kwa kufunga katika mechi nne mfululizo za Ligi Kuu, akiifikia rekodi ya mwisho kufikiwa na Mikel Arteta mnamo 2010.
Mwenendo wa Nidhamu
Everton wamepata jumla ya kadi za njano 21 katika mechi zao sita zilizopita za Ligi Kuu, jambo linaloashiria mtindo wao wa mchezo wa nguvu na ukakamavu mkubwa wanapojiandaa kwa derby hii.
Derby ya Merseyside ni zaidi ya mechi ya kandanda—ni alama ya fahari ya mji, ushindani mkali, na ari isiyovunjika ya vilabu vyote viwili. Iwe ni shangwe za Anfield au uungwaji mkono wa nguvu wa Goodison Park, mchuano huu haukosi kutoa matukio yasiyosahaulika. Timu zote zinapojitayarisha kuingia uwanjani, swali linabaki: nani atajivunia ushindi baada ya filimbi ya mwisho?
